About us: Kuhusu ICR

ISLAMIC CENTRE FOR RESEARCH (ICR) ni kituo cha Kiislamu kilichoanzishwa mwaka 2010 kwa madhumuni ya kuhamasisha maarifa ya Uislamu barabara, kama asemavyo Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’an Tukufu:
“Sema: Hii ndiyo Njia yangu – ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua – mimi na wanao nifuata…” (Qur’an 12: 108)

LENGO KUU:

Kuhamasisha watu wote wau…elewe vizuri Uislamu kwa kutumia hekma, maarifa na mawaidha mazuri.

MAJUKUMU YA ICR:

1. Kutafsiri vitabu kutoka kwenye lugha mbalimbali kuja katika lugha ya Kiswahili ili kuwarahisishia wazungumzaji wa Kiswahili kuuelewa Uislamu na kuufanyia kazi. Hii ni kwa sababu maarifa mengi ya dini yetu yapo katika lugha hizo, na si Waislamu wote wanaozijua hizo lugha na hivyo kuwanyima fursa ya kuyaelewa mazuri ya Uislamu.
2. Kukusanya na kutoa taarifa (information) mbalimbali kuhusu Uislamu na Waislamu.
3. Kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha kazi za da’wah.
4. Kutoa huduma za kibinaadamu kwa jamii.

PROGRAMU ZA SASA:

1. Vitabu vipatavyo 45 vimetafsiriwa kutoka kwenye lugha mbalimbali za kigeni kuja katika Kiswahili tangu kuanzishwa kwa kituo hiki. Bado kazi zinaendelea.
2. Kipindi cha redio kinachorushwa kila siku ya jumanne usiku 3 mpaka saa 4 usiku. Kipindi hiki hudaminiwa na ICR na kurushwa moja kwa moja na idhaa ya Redio Sauti ya Qur’an. Aidha, mipango inafanyika ili kuhakikisha tunapata vipindi katika redio nyingine na kwenye vyombo vya habari vya kawaida. Kipindi hiki hujulikna kwa jina la TUZUNGUMZE UISLAMU, na huzungumzia mambo yote, hususan ya kijamii na kutoa suluhisho la kidini kwa matatizo hayo.
3. Group katika mtandao wa kijamii wa facebook lijulikanalo kama ISLAMIC CENTRE FOR RESEARCH (ICR) lenye wanachama wapatao elfu moja huku wengine wakiendelea kusajiliwa na kuunganishwa kwa ajili ya kupata uzoefu wao na kuwashirikisha katika kutoa elimu na maarifa ya dini yetu tukufu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: